airport jogging club

motto

video

Friday, November 6, 2015

Dk. Kigwangala ataka shirikisho la Jogging


1
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akizungumza na vikundi mbalimbali vya Joging vilivyoshiriki katika tamasha la mbio za Amani lililoshirikisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za nchi na kupokelewa na mbunge huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Dr. Khamis Kigwangala amewaasa wanasiasa kutoleta siasa za uchochezi hasa katika mchakato mzima wa Katiba mpya ambapo amesema waachwe wananchi wenyewe waisome waielewe na wao wataamua kama wataipigia kura ya Ndiyo au Hapana, mapokezi hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
.Ahimiza amani na mshikamano, katiba isiwagawe Watanzania
Na Mwandishi wetu
KLABU za Jogging nchini zimeshauriwa kujiunga pamoja na kuunda shirikisho lao ili ziweze kufanikisha malengo yao ya kimichezo na kiuchumi.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam leo Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mbio maalumu za amani zijulikanazo kama; ‘Jogging for Peace’ ambazo hufanyika kila mwaka chini ya uratibu wa klabu ya Faita Jogging ya Temeke na kushirikisha klabu kutoka mikoa mbalimbali.
Dk. Kigwangala ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tamisemi, alisema awali baada ya kupata mwaliko alikuwa hajui atazungumza nini na wala hakufikiria atakutana na kitu kikubwa kama hicho, lakini amejifunza mengi ikiwemo kuona taifa lenye afya.
“Kwa kweli leo nimejifunza vingi ikiwemo kwamba klabu hizi za Jogging ni jeshi kubwa… katika klabu wakati nawapokea ilikuwa na hamasa na nyimbo zake zenye ujumbe mbalimbali, nimeona makundi ya rika mbalimbali wakiwemo wazee ambao kichwa chote kimejaa mvi, lakini wanashiriki mazoezi, kukimbia kutoka uwanja wa taifa hadi hapa sio mchezo, hivyo nawasihi wake kwa waume ambao bado hawajaanza mazoezi waanze kwani michezo ni afya,” alisema Dk. Kigwangala na kuongeza.
Leo nitawachangia kitu, viongozi wote mliopo hapa, muongoze mchakato wa kuanzishwa Shirikisho la Jogging la Taifa…wako wazee wetu hapa, mkiwatumia Malinzi (Dionis), na Kanali Kipingu (Idd), wana uzoefu katika haya na watasaidia kupatikana usajili haraka na nitagharamia gharama zote za usajili.
2
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akijitolea damu kwa kitengo cha Damu salama ambacho kikilishiriki sambamba na tamasha hilo kuhamasisha wanamichezo hao ili wajitolee damu katika kuokoa maisha ya wahitaji wa damu.
“Jeshi hili linapaswa kujiwezesha kiuchumi na kuiwezesha jamii, mkishaunda Shirikisho anzisheni klabu ya kuweka na kukopeshana, nitawachangia mtaji wa sh milioni 2 kwa vyama vya Zanzibar na milioni 3 kwa bara na milioni moja ya usajili,” alisema Dk. Kigwangala na kushangiliwa na wanamichezo waliojitokeza kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Aidha, alichukua fursa hiyo kuwataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano uliopo hususan wakati huu wa kuelekea kura ya maoni kwa ajili ya Katiba iliyopendekezwa.
Aliyaasa makundi mbalimbali ya wanasiasa, kuacha kauli za uchochezi zitakazowagawa wananchi na kusababisha amani kutoweka, bali wawaache wananchi wenyewe kwa matakwa yao kupiga kura ya hapana ama ndio.
Naye Mwenyekiti wa Faita Jogging, Omar Omar, alisema walianzisha mbio hizo mwaka juzi kutokana na kuona viashiria mbalimbali vya kutoweka kwa amani sehemu mbalimbali ikiwamo mauaji na ukatili kwa vikongwe, walemavu wa ngozi, utupaji vichanga na mengineyo, hivyo wakaona watumie jukwaa lao la jogging kupiga vita.
3
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Alisema mipango yao ya baadaye ni kuyafikia maeneo yaliyokosa amani ikiwamo yaliyoandamwa na mauaji hayo ya vikongwe na baadaye kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Mlezi wa Faita Jogging, Said Mgawe, mbali na kumpongeza Dk. Kigwangala, Mwenyekiti wa BMT aliyemaliza muda wake, Dionis Malinzi na Mwenyekiti wa zamani wa baraza hilo, Kanali mstaafu Idd Kipingu kwa kuhudhuria, aliyapongeza majeshi ya ulinzi na usalama yaliyoko Manispaa ya Temeke kwa mchango mkubwa kwa vijana wao katika kukuza vipaji vyao.
“Tunayapongeza majeshi yaliyoko Temeke, yamekuwa yakiruhusu vijana wetu kuingia kambini na kutumia viwanja vyao, vifaa bure…timu yetu ya Temeke U-17 iliyoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars na kubuka mabingwa iliweka kambi kambi ya Twalipo….Pia Chuo Kikuu cha Polisi kina gym ya kisasa kabisa na vijana wanapata nafasi ya kufanua mazoezi, kwa kweli tunashukuru sana,” alisema Mgawe.
Mbio hizo za amani zilianzia na Uwanja wa Taifa hadi viwanja vya Mnazi Mmoja na kushirikisha klabu mbalimbali ikiwamo Kitambo Nona, Magenge 20 za Zanzibar, Muungano, Mzimuni za Dodoma, Mtoni Relini, Madafu, Msasani, Wasafi, Kindande, Wakali, Home Boys, Polisi Barracks, Wastaarabu, Tandika, Zakhem, Msasani, Machimbo, Home Boys, Navy, Temeke Jogging na nyinginezo.
4
Kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT Bw. Dioniz Malinzi na Bw. Jimmy mmoja wa viongozi wa shirikisho la vyama vya Jogging wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika tamasha hilo.
5
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika mazoezi.
6
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.
7
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja mara baada ya kumaliza mbio za Amani.
8
Bw.Abdulla Mohamed Mwenyekiti wa Mipango ya Maandalizi ya tamasha hilo akimkabidhi jenzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT Bw. Dioniz Malinzi.

9
Mdau wa michezo na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu akizungumza na vikundi hivyo.
10
11
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki kucheza  kigoma cha Amani mara baada ya kupokea vikundi vya Jogging katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
12
Bw. Dioniz Malinzi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo BMT akizungumza jambo na vikundi hivyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Tamasha la Mbio za Amani.
13
Vikundi hivyo vikifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
14
Vikundi hivyo vikiimba wimbo wa Taifa

No comments:

Post a Comment